Burudani

Diva kumleta Alicios Theluji Bongo

Mtangazaji wa Clouds FM, Loveness maarufu kama Diva, kupitia kampuni yake, Divas Events anatarajia kumleta Tanzania kwa mara ya kwanza msanii mwenye asili ya nchini DRC aishiye Kenya, Alicios Theluji.

10406484_1053560447992527_1390617565652046014_n

Diva ameiambia Bongo5 kuwa Alicios atatumbuiza kwenye show kubwa aliyoipa jina ‘Usiku wa Sauti’ huku pia wasanii wakali wa Bongo Flava wakihusika.

“Nimeanza kufanya events kupitia clubs nia ikiwa ni kutengeneza events company yenye entertainment zaidi kwa vijana,” amesema.

“Baada ya kufanikiwa kupitia divas wild events kwa muda nikakaa kutaka kumleta msanii anayependwa na vijana hasa Tanzania, chaguo likaangukia kwa Alicios.”

Mtangazaji huyo amedai kuwa tarehe na mahali itakapofanyika show hiyo atavitaja siku chache zijazo.

Hivi karibuni Alicios aliachia wimbo mpya uitwao Loved by You.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents