Picha

Diva: Naogopa sana kuzaa mtoto, nita adopt mtoto in my life

Unakumbuka Beyonce alivyowahi kusema baada ya kumshuhudia dada yake Solange alipokuwa labour akijifungua miaka kadhaa iliyopita? Well, baada ya kushuhudia alisema hadhani kama ataweza kuzaa kwasababu anaogopa. Lakini mwangalie sasa hivi! She is a proud mother. Mama Blue Ivy. So inaonekana kama madiva wengi wanaogopa sana kuzaa, including Tanzania’s own, Loveness.

Juzi kupitia website yake alijibu barua pepe ya shabiki wake aitwaye Halima Mwinyaka wa Kawe, Dar es Salaam aliyetaka kujua nini Diva huyo anaokiogopa maishani na yeye kusema anaogopa kuzaa. Hivi ndivyo alivyoelezea kwanini anaogopa.

“Halima kuna kitu kimoja nakiogopa sana katika maisha nacho ni kuzaa mtoto. naogopa sana sana kuzaa mtoto. process nzima ya kuwa na mimba yaani tumbo kuwa kubwa kwanza naogopa na naona aibu sana yaani nahisi kwanza nikiwa na tumbo kubwa kabisa la mimba ntakuwa najifungia ndani na sitatoka kabisa mtu anione kitu ambacho kitakuwa kigumu coz its a hustler , kabisa !!

Na naogopa yale maumivu wakati unazaa .. nikiangaliaga movie huwa nalia na nazima tv na kuondoka kabisa eneo hilo naogopa sana kuzaa mtoto ,naogopa pia mama mjamzito huwa natetemeka nikiona mtu ana mimba sana sijaelewa kwanini ila hilo ndilo jambo naogopa sana.Sitaki hata anisogelee , nakumbuka mtu mmoja tu kumshika tumbo lake alikuwa Zamaradi Mketema nikamuuliza, ‘haliumi? akasema haliumi, ‘iko siku na wewe utatamani tu , sasa hivi unasema tu.’ Ila wakati namshika tumbo nilikuwa naogopa natetemeka, huyo ndo mtu wa pekee niliewahi kumgusa tumbo la mimba , sirudii tena yaani maana nilihisi kama namuumiza.

But seriously nimekuwa nikiamini mtoto wa mwenzio pia ni mtoto wako then will go for adoption miaka 3 mbele ntaenda ku adopt mtoto na ntampenda sana as if ni wangu,atakuwa wangu ntampa mapenzi yote tena na zaidi sababu I love children, I love playing with them , I love spending time with them, but mimi kuzaa kabisa kwenda hospital that is a big no no no!! Naogopa sijui nisemeje but GOD IS GOOD In future ntaa adopt mtoto Tuombe Mungu.”

But not so fast Diva………. Ukiolewa na mbongo itabidi uliondoe hilo wazo sababu nyumba haitakalika. Otherwise ukiendelea na msimamo huo, utamlazimisha mumeo aende kutafuta nyumba ndogo amzalishe ili aache photocopy duniani na wewe ukiendelea kuwa busy na adoption. Si jambo baya lakini, tunakuombea upate mwanaume mwelewa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents