BurudaniUncategorized

Dj Khaled aahidi kufanya hili wiki ijayo

Kaa tayari kusikia wimbo mwingine mpya wa Dj Khaled aliomshirikisha rapper Drake.

Khaled ameonekana kuwa na hasira zaidi tangu alipoingia Roc Nation kwa kuachia ngoma mfululizo ikiwemo ‘I’m The One’ aliowashirikisha mastaa kibao na kufanikiwa kujitengenezea rekodi kibao pamoja na kusikilizwa zaidi katika mtandao wa Apple katika wiki yake ya kwanza na kuongoza kwenye chati za Billboard.

Kupitia mtandao wa Instagram, rapper huyo amethibitisha kuachia wimbo wake huo mpya Jumatatu ijayo ambao pia utapatikana katika albamu yake ya ‘Grateful’ ambayo itatoka mwaka huu.

“Also I have very important info Regarding #GRATEFUL THE ALBUM #6AM #Monday ! BE READY!! Have a blessed weekend get some rest!! @wethebestmusic @epicrecords @rocnation,” ameandika Dj Khaled katika moja ya picha za cover alizoweka katika mtandao huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents