Burudani

DJ Khaled aisifu namba 23 katika maisha yake

Ukizungumzia Albamu ya Greatful ya Dj Khaled kwa sasa utakuwa unazungumzia moja ya albamu bora kabisa kwa kipindi hiki zinazofanya vizuri.

     Dj Khaled akiwa na mtoto wake Asad Khaled

Grateful iliyotoka Juni 23 imekuwa moja ya Albamu inayompatia mafanikio makubwa msanii huyo huku namba 23 ikionyesha kuwa ni namba ya bahati na ya mafanikio kwa rapper huyo.

Kwa mujibu wa Khaled mwenyewe ameandika katika mtandao wa Instagram kuelezea umuhimu wa namba hiyo katika maisha yake huku ikimuhusiha kupata mtoto wake wa kwenza mnamo Oktaba 23 mwaka jana.

“MY SON WAS BORN ON oct #23 my album #GRATEFUL came out June #23 Now my ALBUM IS PLATINUM ON AUGUST #23 and And my son turns 10 months today,” he wrote. “And the the album has #23 tracks and I got my own @jumpman23 safe to say #23 is special # .. FAN LUV WE DID IT !!! #DJKHALED #GRATEFUL ALBUM OFFICIALLY PLATINUM!!!!!,” ameandia Khaled.

Mapema mwezi huu ngoma ya ‘Wild Thoughts’ ‘I m the One’ zimeingia mauzo ya platnum huku ngoma ya ‘Shining’ ikiingia katika mauzo ya gold.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents