Burudani

Dj Khaled awa ‘surprise’ wanafunzi wa chuo hiki

Alhamisi ya Mei 16 rapper Dj Khaled alikuwa mingoni mwa wageni waliohudhuria katika mahafali ya wanafunzi wanaomaliza masomo katika chuo cha University of California, Berkeley kwa kushtukiza.

Baada ya kuwasili chuoni hapo wanafunzi wa chuo hiko walipata mshangao kumuona msanii huyo, ambapo pia walipata nafasi ya kuongea maneno machache, na hapo ndipo alipoibua hisia za wanafunzi hao. “Sikuja hapa kufanya tamasha. Nimekuja kusifu wafalme wadogo na malkia kwa kuhitimu leo. Hii ni ajabu. Mimi sikuhitimu mwenyewe, hivyo hiki kitu cha kuhitimu ni cha ukaribu na kwangu pia,” amesema msanii huyo.

“This is so inspiring and such a motivational situation today. They didn’t believe in me at one time in my lifetime, but I had to bet on myself and look at me now. I’m on the stage with young kings and queens and the generation of geniuses that’s gonna run the world…They don’t want us to graduate, so we gon’ graduate!,” ameongeza.

Rapper huyo anatarajia kuachia albamu yake mpya mwaka huu iliyopewa jina la ‘Grateful’ ambayo imewakutanisha mastaa kibao wakubwa duniani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents