Burudani

Dj Khaled hakukata tamaa kumsaka Rihanna

Mwanamuziki na mtayarishaji wa muziki nchini Marekani Dj Khaled, amedai kuwa hakuchoka kumtafuta mrembo Rihanna ambaye amekuwa na nyota ya kupenda na watu wengi katika ulimwengu wa burudani.

Kupitia mtandao wa Instagram Dj Khaled ameweka picha akiwa na mrembo huyo na kuandika “#TBT #DJKHALED @badgalriri ……. I never gave up !!! And now we have #WILDTHOUGHTS ! GRATEFUL !.”

Dj Khaled anaweza kujivunia mafanikio aliyoyapata katika albamu hiyo iliyouza zaidi ya kopi laki tano na iliyofikisha mauzo ya Gold, Grateful iliyotoka mwezi Juni 23 mwaka huu ikiwa na nyimbo takribani 23 huku watu kama Jay Z, Beyonce, Alcia Keys, Nas, Travis Scott, Niki Minaj, Chance The Rapper na wengine, wakihusika kushiriki.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents