DStv Inogilee!

DJ Mafuvu akutana na mazito Clouds FM, adai DJ Zero, Sinyorita na D-Ommy wanamzibia riziki

Moja kati ya Ma DJ pendwa nchini Tanzania, DJ Mafuvu amefunguka kuwa uongozi wa Clouds Media Group upo tayari na umeridhia kuendelea kufanya naye kazi lakini baadhi ya wafanyakazi wa kituo hicho ndio wanaomfanyia figisu figisu.

Akielezea kwa hisia kupitia ukurasa wake wa Instagram, DJ Mafuvu amewataja watu hao wanaomfanyia figisu figisu hizo kuwa ni DJ D-Ommy, DJ Zero, DJ Sinyorita, DJ Bulla na DJ Feruu.

Najua my Fans n’ Supporters (Mashabiki) ndio mmekuwa mstari wa mbele kunisukuma sana kuhusu kurudi Media, na Uongozi wa Clouds Media Group (CMG) ukanipa ile nafasi na wangependa niendelee kuwapa burudani lakini inabidi tu niweke wazi kuhusu hii ishu na niwachane tu hawa Jamaa; @djzeroxxl@djdommy @djsinyorita @djbullatz@djferuuh acheni kufanya figisu chini chini mchongo usifanikiwe, halafu wakumbuke haya Maisha tu tuache kuwekeana giza kindezi! Ila najua hawajui tu kama wanashindana na nguvu ya Umma… Na kama walikuwa hawana habari waambieni kabisa “Nimeagizwa na Mashabiki kurudisha hii burudani kwenye Masikio yao na si vinginevyo” Let’s get real! Hivi kwani haiwezekani kuishi peaceful bila fitina!? Anyways, Mashabiki walionihitaji kurudi huku watawapa darasa vizuri! Period!

DJ Mafuvu wiki mbili zilizopita alipata nafasi ya kama mgeni mualikwa kwenye kipindi cha XXL na alipiga show kali sana iliyoamsha wafuatiliaji wa kipindi hicho pendwa cha burudani nchini Tanzania.

Hata hivyo, habari njema ni kuwa tayari Idara ya Muziki ya Clouds FM kupitia kipindi cha XXL, imetangaza kuwa kesho DJ Mafuvu atakuwepo kwenye kipindi cha Leo Tena.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW