Michezo

Djokovic amshinda Andy Murray mashindano ya Australia Open

Mchezaji tenis nambari moja duniani kwa upande wa wanaume Novak Djokovic ameibuka mshindi wa taji la Australia Open baada ya kumshinda Andy Murray.

30C0DEFF00000578-3425004-image-a-51_1454237042433

MSerbia huyo mwenye umri wa miaka 28 alipo mshinda Murray seti tatu kwa nunge za alama 6-1 7-5 7-6 (7-3).

Kichapo hicho ni cha 5 kwa muingereza Murray ambaye sasa ameshindwa katika fainali zote 5 alizowahi kushiriki za mchuano wa wazi wa Australia.

4 kati ya hizo mikononi mwa mtani wake wa jadi Djokovic

Djokovic huu unakuwa ni ushindi wake wa 6 mjini Melbourne na sasa anatoshana nguvu na bingwa wa zamani Roy Emerson kutoka Australia.

Murray, 28, sasa ameingia katika kumbukumbu kwa kushindwa katika fainali 5 za Grand Slam za tenis tangu kuasisiwa kwa mashindano hayo ya wazi mwaka wa 1968.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents