Michezo

Djokovic amshinda Federer na kuingia fainali ya mashindano ya Australian Open

Mchezaji nambari moja duniani katika mchezo wa tenisi Novak Djokovic amefuzu kucheza fainali ya mashindano ya Australian Open kwa mara ya sita baada ya kumfunga Roger Federer.

30A8339F00000578-0-image-a-11_1453976142552

Mchezaji huyo amepata ushindi wa 6-1 6-2 3-6 6-3.

Djokovic alitawala seti mbili za kwanza, lakini baada ya muda Federer alianza kujikwamua.

30A8FFB800000578-0-image-a-7_1453974884075

Hata hivyo, Djokovic alifanikiwa kushinda seti ya mwisho.

Djokovic atakutana na Mwingereza Andy Murray au raia wa Canada Milos Raonic kwenye fainali.

Mserbia huyo amemshinda Murray kwenye fainali mara tatu awali, ikiwa ni pamoja na mwaka jana aliposhinda kwa seti nne.

“Nilicheza vyema sana seti mbili za kwanza lakini ilinibidi kwa sababu Roger amekuwa akicheza vyema sana na nilijua angekuwa mkali,” amesema Djokovic baada ya ushindi wa leo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents