Habari

Dk. Remmy kuipua albamu ya pili

Dk RemmyMWANAMUZIKI mahiri aliyetamba zamani katika muziki wa dansi nchini kabla ya kuokoka, Dk. Remmy Ongala, yuko mbioni kuipua albamu yake ya pili ya nyimbo za Injili itakayojulikana kwa jina la ‘Maisha Yangu kwa Yesu’.

Dk Remmyna Abdilahi Daudi


 


MWANAMUZIKI mahiri aliyetamba zamani katika muziki wa dansi nchini kabla ya kuokoka, Dk. Remmy Ongala, yuko mbioni kuipua albamu yake ya pili ya nyimbo za Injili itakayojulikana kwa jina la ‘Maisha Yangu kwa Yesu’.


Akizungumza nyumbani kwake, Sinza jijini Dar es Salaam juzi, Dk. Remmy alisema kuwa albamu hiyo itakuwa mitaani mwanzoni mwa mwezi ujao.


Dk. Remmy alisema, albamu hiyo itakayobeba nyimbo 10, tayari iko kwenye hatua za mwisho, katika studio za FM chini ya mtayarishaji Double B.


Alisema, katika albamu hiyo, atavishirikisha baadhi ya vikundi vya dini, likiwamo kundi lake la ‘Imani Group’.


Alipoulizwa kwanini amegeukia muziki wa Injili badala ya ule wa dansi, Dk. Remmy alisema, ameamua kufanya hivyo kwa vile kwa sasa yeye ni mtu mpya, hivyo ameachana na nyimbo za kidunia.


“Nimerudi kwa Mungu na kuacha mambo ya kidunia baada ya kubaini kwamba, nilikuwa katika mstari usiostahili,” alisema.


Alisema, kwa sasa hana budi kutunga nyimbo za kumtukuza Mungu, ili kuutangaza utukufu wake ikiwa ni sehemu ya ushuhuda wake kwa makuu aliyotendewa na Mungu.


Alisema albamu hiyo itakuwa ya pili kuitoa, tangu alipoachana na muziki wa dansi na kurudi kwa Mungu. Albamu yake ya kwanza ilijulikana kwa jina la ‘Narudi kwa Yesu’ aliyoitoa mapema mwaka jana.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents