Dk. Shein kujadili Muungano

Makamu wa Rais Mh Dtk Ali M. Shein, anatarajia kuongoza kikao kitakachofanyika jijini Dar Es Salaam siku ya Alhamisi wiki hii kwa nia ya kujadili masuala mabali mbali ya Muungano

Makamu wa Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dtk Ali Mohammeid Shein


 


Evelyn Mkokoi DSM



Makamu wa Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dtk Ali Mohammeid Shein, anatarajia kuongoza kikao cha Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kitakachofanyika jijini Dar Es Salaam siku ya Alhamisi wiki hii kwa nia ya kujadili masuala mabali mbali ya Muungano.



Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi mwenye dhamana ya Kushughulikia masuala ya Muungano kutoka katika Ofisi ya Makamu wa Rais Muheshimiwa Mohammeid Seif Khatib, katika kikao na wanahabari kilichofanyika Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.



Mh. Khatib amesema kuwa, baadhi ya Mambo yatakayojadiliwa ni pamoja na kupata taarifa ya utekelezaji wa masuala mbali mbali ya Muungano , Namna ya kushugulikia Mapato ya Mafuta na Gesi Asilia na jinsi ya kutatua suala la wafanyabiashara kutozwa kodi mara mbili.



Akijibu swali la mwanahabari kuhusu suala la wapemba kutaka kujitenga, Mh Khatib alieleza kuwa si suala la wapemba wote bali ni baadhi tu ndiyo wanataka kufanya hivyo na , aliongeza kwa kusema kuwa ni lazima tuwe na umoja na mshikamano ili tujenge Tanzania yetu, “Sidhani kama tunaweza kuishi kwa Kutengana Alisema.”



Akifafanua kuhusu suala la Muafaka, Mh. Khatib alisema, Hilo si suala linaloshughulikiwa na Ofisi yenye dhamana ya masuala la Muungano bali ni suala la vyama vya siasa.



Kikao hicho ni moja ya vikao vilivyoagizwa na Serikali ya Awamu ya nne katika kuhakikisha kuwa vikwazo katika utekelezaaji wa masuala ya Muungano vinatatuliwa chini ya usimamizi wa Makamu wa Rais.


 


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents