Habari

Dk. Sheni: wazawa wapewe kipaumbele

SERIKALI imewataka wawekezaji nchini kutoa kipaumbele kwa wazalendo katika suala la ajira kwenye miradi yao.

SERIKALI imewataka wawekezaji nchini kutoa kipaumbele kwa wazalendo katika suala la ajira kwenye miradi yao.


Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa hoteli makazi inayomilikiwa na Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF) mjini hapa jana, Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein, alisema imekuwa ni tabia ya baadhi ya wawekezaji kungÂ’angÂ’ania kuajiri wageni bila ulazima badala ya wenyeji.


Dkt. Shein aliongeza kuwa baadhi ya waajiri wameonesha pia kiburi kwa kudharau wafanyakazi wenyeji na kuwaona kuwa hawafai na aliwataka kuajiri wageni pale tu itakapothibitika kuwa hakuna Mtanzania mwenye sifa ya kufanya kazi hiyo.


Sambamba na mwito huo, aliwakumbusha wawekezaji wakiwamo wenye hoteli kuhakikisha kuwa wanatumia bidhaa za ndani badala ya kuagiza za nje ya nchi ambapo alifafanua kuwa kuendelea kuagiza bidhaa nje hakujengi uhusiano mzuri kati ya miradi ya uwekezaji na wenyeji.


Mradi huo wa hoteli makazi ambao una jumla ya vyumba 40 utatoa huduma mchanganyiko ambapo wageni watakuwa na hiari ya kuchagua kujihudumia wenyewe au na hoteli baadhi ya huduma kama vile chakula.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents