Burudani

DKB aandika barua ya kuomba msamaha


Baada ya kutolewa kwenye shindano la Big Brother Africa kutokana na kuvunja sheria za mashindano hayo, aliyekuwa mwakilishi wa Ghana, DKB ameiandikia barua BBA kuomba msamaha.

“Watu wazuri wa Africa, kuna mambo mengi natamani ningefanya kusawazisha tukio hili baya lakini kama sote tujuavyo, mtu hawezi kurudi katika muda uliopita.

Nilikuwa na muda katika maisha yangu wa kuifurahisha Africa kwenye jukwaa muhimu lakini niliuharibu kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu.

Nipo hapa kuomba radhi kwa waafrika wote, kwa watu wa nchini yangu Ghana, timu nzima ya Big Brother Africa, washiriki wenzangu na hasa kwa Zainab na familia yake.

Ninawajibika kikamilifu kwa matendo yangu na kwa namna yoyote ile sihalalishi kitendo cha kumpiga mwanamke hata kama uchokozwe vipi.

Kwa watazamaji wangu wapendwa, mashabiki na wakosoaji, nasema asanteni kwa ushirikiano wenu. Ninaomba mnisamehe kwa kuwaangusha na ninaahidi kuwa sitarudia tena tabia ya kijinga kama hiyo.

Hilo ni ombi langu la kweli la msamaha na naamini limepokelewa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents