Habari

Dkt. Abiy Ahmed ashinda uwenyekiti EPRDF, akaribia kuwa Waziri Mkuu Ethiopia

Umoja wa chama cha EPRDF nchini Ethiopia kimemchagua Dkt. Abiy Ahmed kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa asilimia 60.

                                                           Dkt. Abiy Ahmed

Wakati huo huo imedaiwa kuwa Dkt. Abiy anaweza kukalia kiti cha Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo ambacho kwa sasa kipo wazi kilichoachwa na Hailemariam Desalegn aliyetangaza ghafla kujiuzulu mwezi uliopita.

Kiongozi huyo mpya wa EPRDF ameshinda nafasi hiyo kwa kura 108 kati ya 180 katika mkutano wa Halmashauri ya EPRDF, ambao unajumuisha wanachama 45 kutoka kila chama kati ya vyama vya siasa vinne vinavyonda umoja huo.

Ahmed anatoka katika kabila kubwa zaidi nchini Ethiopia la Oromo ambalo limekuwa likifanya maandamano ya kuipinga serikali tangu mwaka 2015. Siku chache zilizopita alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama cha Oromo People’s Democratic Organisation (OPDO).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents