Habari

Dkt John Magufuli atangazwa Rais Mteule wa Tanzania

Baada ya mvutano mzito wa kampeni na kisha kufanyika uchaguzi wa rais wenye upinzani mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya Tanzania, tume ya taifa ya uchaguzi, NEC Alhamis hii imemtangaza mgombea wa CCM, Dokta John Pombe Magufuli kuwa mshindi wa nafasi ya urais.

20151029104052
Rais anayeondoka madarakani, Jakaya Kikwete akimpongeza Dokta John Magufuli mara baada ya kutangazwa mshindi wa kinyang’anyiro cha urais. Wawili hao walikuwa ikulu kufuatilia matangazo ya moja kwa moja kupitia televisheni

Ushindi huo unamfanya Magufuli kuwa rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na akiapishwa atakuwa rais wa awamu ya tano. Magufuli atachukua nafasi ya Rais Jakaya Kikwete aliyeongoza kwa mihula miwili.

3
Rais Jakaya Kikwete na mke wake Mama Salma wakimpongeza Dokta Magufuli ikulu ya Dar es Salaam Alhamis hii

Ikitangaza matokeo hayo, NEC imedai kuwa Magufuli amepata jumla ya kura 8,882,935 sawa na asilimia 58.46 na kumzidi mpinzani wake wa karibu, Edward Lowassa wa CHADEMA aliyepata kura 6,072,848 sawa na asilimia 39.97.

20151029104050
Magufuli akiongea na mgombea wa Urais ACT, Anna Mghwira aliyempigia simu kumpongeza

Mgombea wa Urais kwa tiketi ya chama cha ACT, Anna Mghwira amempigia simu kumpongeza Magufuli kwa ushindi huo.

“Mshindi wa kura za urais kwa mwaka huu wa 2015 ametangazwa kuwa ni ndg John Magufuli. Nimempigia simu na kumpa hongera. Amenipongeza kwa kuendesha kampeni za kisayansi. Nina matumaini kuwa Tanzania itakuwa sehemu bora ya kuishi na fahari ya watanzania chini ya uongozi wake,” ameandika kupitia Facebook.

Kwa sasa kilichoki ni kuapishwa tu kwa Magufuli na kuwa rais wa awamu ya tano.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents