Habari

Dkt Kigwangalla amtumbua Mkurugenzi wa wanyama pori

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamisi Kigwangalla amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa wanyamapori wa hifadhi ya Serengeti, kwa tuhuma za kuhujumu Serikali kwa kutoa taarifa za siri za Serikali kwa vyombo vya habari na kutunga taarifa zenye kulenga kuchochea mgogoro wa Loliondo.

Akizungumza katika Hifadhi ya Serengeti, ambapo amefanya ziara ya kushtukiza na kuuzunguka mpaka wote wa Mashariki ambapo hifadhi ya Serengeti inapakana na Pori Tengefu la Loliondo, lenye mgogoro wa muda mrefu.

Dkt. Kigwangalla ameagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudence Milanzi, kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Wanyama Pori, Prof. Alexander Songorwa mara moja. Kwasababu zifuatazo:

1. Tuhuma za kuhujumu Serikali kwa kutoa taarifa za siri za Serikali kwa vyombo vya habari na kutunga taarifa zenye kulenga kuchochea mgogoro wa Loliondo. (Juzi usiku zilizunguka taarifa kwamba Dkt. Kigwangalla yupo na msafara wa gari mbili binafsi (private) njiani kwenda Loliondo na kwamba atalala Hotel ya Acacia iliyopo Karatu. Na leo msafara wake umekuwa ukifuatiliwa na watu wasiojulikana ambapo kila hatua aliyofikia ilikuwa ikiripotiwa kwenye mtandao, hali ambayo imetishia usalama wa kiongozi huyo).

2. Waziri Kigwangalla amesema Mkurugenzi huyo amekuwa akifanya kazi kwa maelekezo ya muwekezaji wa Kampuni ya Utalii wa Uwindaji ya OBC (maarufu kama kampuni ya kiwindaji ya wafalme wa Dubai). Kampuni hii imekuwa ikihusishwa na kashfa kwa miaka zaidi ya 26.

3. Aidha Prof. Songorwa amekuwa akihusishwa na kashfa ya kushiriki kugawa vitalu vya uwindaji kinyume cha sheria. Wiki mbili zilizopita Waziri Kigwangalla alisitisha mchakato wa kuhuisha leseni za uwindaji uliofanywa na Prof. Jumanne Maghembe, aliyekuwa waziri wa Maliasili na Utalii kwa tuhuma za rushwa na kukosekana uwazi kwenye mchakato huo. Pia ameelekeza mchakato wa kugawa vitalu sasa ufanywe kwa njia ya mnada.

Aidha Dkt Kigwangalla ameelekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) waanze kuchunguza kashfa za rushwa dhidi ya kampuni ya OBC na waanze kwa kumhoji bwana Mollel (Mkurugenzi wa OBC) ambaye amekuwa akijigamba kila kona kuwa alimhonga Maghembe dola 200,000, huyu kijana Kigwangalla dola 100,000 inamtosha.

Dkt. Kigwangalla amesisitiza ahongeki na ndiyo maana jitihada za bwana Mollel kumuona zimekwama, na hata alipotumiwa ujumbe kupitia watu wake wa karibu alikataa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents