Habari

Dkt Kikwete amtembelea Kardinali Pengo

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt Jakaya Kikwete amemtembelea Mhadhama Polycarp Kardinali Pengo, nchini Dubai.

Dkt Kikwete ameandika hayo leo, kuwa amemkuta Kardinali Pengo akiwa mwenye siha njema.Dkt Kikwete ametweet kupitia ukurasa wake wa tweeter hivi:

“Nikiwa Dubai safarini kwenda Canada, nimemtembelea asubuhi hii Mhadhama Polycarp Kadinali Pengo na nimefarijika kumkuta akiwa na siha njema.”

Hata hivyo Dkt Kikwete amesema amemtembelea Kardinali Pengo wakati akiwa safarini kuelekea Canada.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents