Michezo

Dkt. Kikwete na Waziri Nchemba waongoza Watanzania mazishi ya Athuman Chama (+Picha)

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mh. Mwigulu Lameck Nchemba hii leo wamewaongoza viongozi wa klabu ya Yanga, wanachama, mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu nchini katika mazishi ya aliyekuwa beki wazamani wa timu na Taifa Stars, Athuman Juma Chama aliyezikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.

Katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Waziri Mwigulu ameelezea namna alivyoshiriki katika mazishi hayo.

Nimeshiriki mazishi ya mchezaji wa Timu ya Taifa wa zamani Marehem Athman Juma Chama.

Tunamuombea apumzike kwa Amani.

Chama ambaye aliichezea klabu ya Yanga miaka ya 80 na kujizoelea umaarufu mkubwa alifariki dunia Jumatatu usiku baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kiharusi na kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa muda wa wiki mbili.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents