Habari

Dkt. Migiro akerwa na ukatili,utumiaji nguvu kwa wanawake

NAIBU Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha Rose Migiro, ameeleza kukerwa kwake na vitendo vya utumiaji nguvu dhidi ya wanawake na wasichana vimeenea sehemu zote.

NEW YORK, Marekani

 

NAIBU Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha Rose Migiro, ameeleza kukerwa kwake na vitendo vya utumiaji nguvu dhidi ya wanawake na wasichana vimeenea sehemu zote.

 

Dkt. Migiro alisema hayo juzi wakati akizungumza na tume ya umoja ambapo alieleza kuwa vitendo vimeenea sehemu zote.
“vitendo hivi hufanywa na ndugu na wanafamilia, watu wasiofahamika na mawakala wa Serikali ulimwenguni kote, katika maeneo ya hadharani na faragha, wakati wa amani na wakati wa vita.”alisema Dkt. Migiro

 

Naibu Katibu Mkuu huyo aliitaka Tume hiyo ichukue hatua muhimu ili kuboresha maisha ya wasichana ulimwenguni kote.

 

Dkt. Migiro pia alitoa mwito kwa Serikali mbalimbali, jamii na taasisi za kimataifa kusaidia katika kukomesha usafirishaji wa binadamu.

 

“Ukweli ni kwamba kuna namna ya utumwa unaoendelea katika dunia ya leo, suala ambalo ni aibu. Nikiwa kama mwanamke wa kiafrika, nipatwa na huzuni,” alisema Dkt. Migiro Jumatatu wiki hii katika mkutano wa kimataifa kuhusu usafirishaji wa wanawake na watoto.

 

Naibu Katibu Mkuu huyo alipendekeza kwa mataifa kuungana na Mkakati wa kupambana na usafirishaji binadamu na biashara ya utumwa, ambao ni mpango mpya wa UN unaotarajiwa kuzinduliwa mjini Vienna, Austria mwaka huu.

 

Biashara ya binadamu inayolenga kuwanyonya kwa njia ya kuwatumikisha kazi au biashara ya ngono, imekuwa ikiwaingizia watu mabilioni ya dola.

 

Mwishoni mwa mwezi huu, takribani wawakilishi 1,000 wa Serikali mbalimbali na wale wa taasisi binafsi wanatarajia kuhudhuria mkutano Abu Dhabi, utakaojadili ukomeshaji wa biashara ya binadamu, kwa kuungwa mkono na Ofisi ya UN inayohusika na dawa na uhalifu.

 

Wakati huo huo, Balozi Patricia wa Marekani amesema, Marekani imejitolea kuwalinda , kuwaendeleza na kuwawezesha wanawake wa Marekani na ulimwenguni kote.

 

Balozi huyo alisema juzi kuwa mtazamo wa Marekani kuhusu wanawake na wasichana yanahusishaa ustawi na maendeleo ya wanawake ulimwenguni kote.

 

Alisema, nchi hiyo inafadhili miradi mingi ulimwenguni kote ya kuwasaidia wanawake na wasichana hasa wale wanaoishi katika mazingira magumu.

 

Ofisa huyo wa Marekani alisema, Marekani inafadhili miradi kadhaa ya kukabiliana na vitendo vya utumiaji nguvu dhidi ya wanawake, ikiwa ni pamoja na mpango wa dola milioni 15 wa kupambana na vitendo vya nguvu dhidi ya wanawake jimboni Darfur.

 

Alisema mpango huo unatoa misaada ya kibinadamu pamoja na kuunga mkono haki za binadamu.

 

Mpango mwingine wa nchi hiyo ni wa kuboresha elimu, ambapo nchi hiyo itatoa ufadhili kwa waanfunzi wasichana 550,000 wa shule za msingi na sekondari katika nchi 40 za kiafrika.

 

Alisema kupitia misaada hiyo, watoto zaidi ya milioni tano, theluthi moja kati yao wakiwa wasichana wanaosoma nchini Afuganistani.

 

Inaelezwa kuwa takribani wasichana milioni 55 wananyimwa fursa za kwenda shule, na mamilioni ya wasichana wenye umri wa kwenda shule wanafanya kazi za ndani. vile vile asilimia 40 ya askari ni wasichana kwa mujibu wa Tume inayoangalia Hali ya Wanawake (CSW). (USIS)

 

Source: Majira

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents