Dkt. Nchemba awakemea wanasiasa wanaoihusisha serikali na shambulio la Mh. Lissu

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amewataka wanasiasa kuacha kutumia kuumia kwa Mbunge Tundu Lissu kama chambo ya kisiasa katika majukwaa.

Dkt. mwigulu amesema hayo mkoani Singida wakati wa kampeni za udiwani kata ya Mitunduluni.

Aidha Dkt Mwigulu amewataka waache kutumia matatizo ya ndugu yao kama mitaji ya kisiasa badake yake waje na hoja za maana za kusaidia katika maendeleo ya nchi.

Aliongeza kusema kuwa mwaka uliopita uhalifu wa ajabu ulitokea ambapo kuna watoto wadogo wa chekechea walitekwa na kuuwawa ambao hawakuwa na hata shida na mtu yoyote na wazazi wao ni watu wa kawaida kabisa je serikali ndio imehusika.

“Sisi tunaoshughulika na masuala ya uhalifu tunatafuta wahalifu wanaofanya msuala ya kihalifu, kuna watu wanaona ni ajenda ya kisiasa wakati sisi tuombea mtu apone” alisema Dr Mwigulu

DKt. Mwigulu ameongeza kusema kuwa je angeamua kuendelea kusema kuhusu kupigwa risasi kwa mwanajeshi masaki inauhusiano gani na shida za kata ya mitundulini, hivyo wananchi wa singida wawaadhibu kwa kuwanyima kura katika uchaguzi wa tarehe 17 mwezi huu.

Uchaguzi mdogo katika kata ya mitunduluni unafanyika baada ya Diwani aleyekuwepo katika kata hiyo kufariki dunia kwa maradhi.​

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW