Habari

Dkt Shein awaomba wananchi kuheshimu maamuzi ya serikali

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi, Dkt. Mohamed Shein amewataka wananchi kuheshimu mipango ya serikali katika masuala ya uwekezaji kwasababu yana tija kwa maendeleo ya wananchi na serikali.

dsc_1958

Akizungumza alivyotembelea ujenzi wa mji wa kisasa na makazi Funga na kuangalia mradi wa hoteli Mtoni, Dkt Shein alisema serikali imetenga maeneo mengi ya uwekezaji na amesema wananchi hawapaswi kuyatumia kwa shughuli zingine.

“Nataka nitoe wito kwa wananchi waunge mkono jitihada za serikali za kubadilisha mazingira na maendeleo ya Zanzibar, tunapowaambia ardhi hii tumeitenga kwa wawekezaji, wasije wao tena kuja kupachika pachika miti yao na makuti yao, wacha serikali itekeleze mpango uliokusudia,” alisema.

“Wapo wengine tunapojenga na wao wanakuja kujenga na ndiyo maana juzi tukavunja zile nyumba za Funga, hawakutakiwa wajenge pale,sasa tumelipima eneo hili kwaajili ya uwekezaji, kwahiyo wananchi waheshimu maamuzi ya serikali yao,” alisisitiza Dkt Shein.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents