Dkt Shein Mgeni Rasmi Siku Ya Mazingira Duniani

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Ali Mohammeid Shein, anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, yatakayo adhimishwa kitaifa Juni Tano Mwaka huu Mkoani Shinyanga

Evelyn Mkokoi


Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Ali Mohammeid Shein, anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, yatakayo adhimishwa kitaifa Juni Tano Mwaka huu Mkoani Shinyanga.



Akiongea na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Habari Maelezo kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Masuala ya Mazingira, Mh Dkt Batilda Burian, Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Erick Mugurusi amesema kuwa, Kauli mbiu ya Maadhisho hayo mwaka huu kitaifa inayosema “Hifadhi Mazingira: Dhibiti Uchomaji Moto, Panda Miti.” Inalenga kuelimisha na kuhamasisha wananchi vijijini na mijini kuepuka na kudhibiti uchomaji moto wa misitu na uoto wa asili, ukataji miti kiholela na uchafuzi wa Mazingira.



Aidha, Bwana Mgurusi aliongeza kwa kusema kuwa Ujumbe huu pia huenda sambamba na utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Mazingira, Sheria ya Usimamizi wa Mazingira na Mkakati wa Kuhifadhi Mazingira ya Ardhi na vyanzo vya Maji.



Akifafanua zaidi kuhusu lengo kuu la Maadhimisho hayo Kitaifa, Bwana Mgurusi amesema kuwa, Ni jukumu la Serikali na kila Mwanachi kuweka mkazo kuhusu wajibu wa kila mmoja kuhifadhi Mazingira na kuhamasisha kila mwananchi awe wakala mzuri wa jukumu hilo.”Suala la Mazingira ni pana na linamgusa kila mwananchi, hivyo juhudi za kuhamasisha jamii nzima kuhusu hifadhi ya mazingira ni suala lenye umuhimu ulio wazi , Alisisitiza.”



Zaidi ya nchi 180 ikiwemo Tanzania, huadhimisha siku ya Mazingira Duniani, Maadhimisho ya siku hiyo Kitaifa mwaka huu, yataambatana na shughuli mbali mbali zikiwemo za kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira katika maeneo maeneo mbali mbali.


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents