Burudani

Dkt. Shika ni mpango wa Mungu kuwepo – Kala Jeremiah

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Kala Jeremiah amesema’Bilionea’ Dkt. Luis Shika ambaye wiki iliyopita alitangaza kununua nyumba za kifahari za mfanyabiashara Said Lugumi ni mpango wa Mungu.

Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Vijana’ ametumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kueleza jinsi alivyoweza kumuelewa Dkt. Shika kwa kipindi kifupi na kuitaka jamii kumsaidia kutokana na yale aliyopitia.

nIMESIKILIZA KWA MAKINI SANA MAELEZO YA MZEE WETU. SITAKI KUONGELEA UTAJIRI WAKE WALA UMASIKINI WAKE NATAKA KUONGELEA MAJARIBU ALIYOKUTANA NAYO KATIKA SAFARI YA MAISHA YAKE. NI WAZI KUWA MZEE HUYU YUPO DUNIANI KWA KUWA MUNGU KAMCHAGUA NA MUNGU HUMCHAGUA MTU KWA KUSUDI LAKE. NIONAVYO MIMI MZEE HUYU NI BARAKA KUTOKA KWA MUNGU HAIJALISHI MADHAIFU YAKE ILA KWA UHAKIKA NI MPANGO WA MUNGU KUWEPO KWAKE KWETU. NIWAOMBE WANAJAMII TUMUONEE HURUMA NA TUMPENDE HICHO NDICHO KITU PEKEE ANACHOHITAJI MZEE HUYU NA KWA HAKIKA AMEKIKOSA KWA MIAKA MINGI. HAITAKUGHARIMU CHOCHOTE KUMHURUMIA NA KUMPENDA. NAWAOMBA. 🙏🙏🙏🙏
#KIJANA

Umaarufu wa Dkt. Shika umekuja baada ya kujitokeza katika mnada ulifanywa na Kampuni ya Udalali ya Yono kwa amri ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuuza nyumba za Lugumi ambapo Dk. Shika aliahidi kununua nyumba hizo kwa thamani ya Sh bilioni 2.3 lakini alishindwa kulipia asilimia 25 ya fedha hizo ambazo ni shilingi milioni 800 kitu ambacho kilipelekea akamatwe na polisi kwa kosa la kuharibu mnada na utapeli lakini sasa yupo nje kwa dhamana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents