Burudani

DMX apelekwa rehab mjini California

Hali ya afya ya DMX imezidi kuwa mbaya.

Kwa mujibu wa chanzo cha mtandao wa TMZ, rapper huyo mwenye miaka 46 amepelekwa rehab mjini California, kwa ajili ya kuweza kupata uangalizi wa kuachana na matumizi ya pombe kali pamoja na madawa ya kulevya.

Ushauri huo wa kwenda katika kituo hicho ulitoka kwa meneja wake Pat Gallo, na aliyekuwa mke wake, Tashera Simmons.

Wiki hii DMX, alivunja show zake tatu alizotakiwa kutumbuiza huku akishindwa kufanya vizuri katika show ya wikiendi iliyopita katika ukumbi wa Brooklyn’s Barclays Center akiwa na kundi lake la Ruff Ryders.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents