Habari

DNA Arejea tena kwa muziki wa ‘Kidunia” baada ya kuokoka


Msanii wa zamani wa kapuka ambaye baadaye aligeukia muziki wa injili nchini Kenya, DNA, ameamua kurejea tena kwenye muziki wa kidunia (secular music).
Hata hivyo wokovu wake uko pale pale.
DNA (Dreams N Ambitions) alitamba sana mwaka 2006 kwa club banger, Banjuka, ambayo mpaka leo hii ikipgwa watu ni ‘kubanjuka’ tu.
Baadaye rapper huyo aliamua kuokoka na kurekodi wimbo uitwao Mtoto Wa Sonko kuelezea maisha mapya ya wokovu.
Hata hivyo baada ya kukaa kwa muda amekuja kugundua kuwa hawezi kujibana kwenye muziki wa injili peke yake.
DNA alitangaza uamuzi huo wa kurudi kwenye game kwa kuzungumza na waandishi wa habari ambapo hata hivyo hakujibu maswali yaliyohusu imani na familia.
Alieleza kuwa amelijadili suala hilo na familia kabla ya kuamua kuchukua uamuzi huo.
Msanii huyo alieleza kuwa bado ameokoka na harudi kufanya mambo yaliyomharibu miaka iliyopita.
Wimbo wa kwanza kutoka baada ya tangazo hilo unaitwa Maswali Ya Polisi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents