Habari

DODOMA: Bunge laanza rasmi leo, Wabunge waanza kutumia VISHIKWAMBI

Leo Mkutano wa 17 wa Bunge vikao vyake vinaaza rasmi, Bunge hilo pia linaaza kutumia mtandao, Mfumo ambao utapunguza gharama zilizokuwa zikitumiwa kwenye uchapishaji wa nyaraka mbalimbali kutoka Tsh bilioni 1.2 hadi Sh milioni 200 kwa mwaka.

Akizungumza kuhusu wabunge kukabidhiwa na kupewa maelekezo ya matumizi ya Tablets (vishikwambi), Katibu wa Bunge, Stephen Kigaigai amesema mfumo huo utaokoa fedha za serikali zilizokuwa zikitumiwa na Bunge.

Kutokana na mabadiliko hayo, Kagaigai amesema Wizara husika zitatakiwa kuja na karatasi kiasi kwa ajili ya kumbukumbu za kiofisi.

Tumezitaka Wizara zinazohusika kuja na na karatasi kiasi kwa ajili ya kumbukumbu za ofisi hususani kwa ajili ya maktaba na baadhi ya maeneo, Kwa hiyo kwa kesho tunaanza Mpango wa Serikali nadhani tutakuwa na nakala ambazo hazitazidi 10 wakati zamani walikuwa wakileta nakala 500,“ameeleza Kagaigai kwenye mahojiano yake na gazeti la Habari Leo.

Kagaigai amesema wamenunua Tablets 450 zenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 900 ambazo zitagawiwa kwa wabunge na makatibu wa bunge na zitatumika katika vikao vya Bunge na kamati zake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents