Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Dodoma: Mgombea TFF ashindwa kujibu swali

Mgombea nafasi ya ujumbe wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),  kutoka kamati ya Utendaji Kanda ya sita yenye mikoa ya Katavi na Rukwa, Baraka Mazengo amejikuta akichemka kujibu swali aliloulizwa na mpiga kura.

 

Wakati wakinadi sera zao kwa mara ya mwisho mbele ya wajumbe Mazengo alishindwa kujibu swali alilotakiwa ataje vyama vinne vilivyomo kwenye mikoa ambayo yeye anaomba kuiwakilisha endapo atapata ridhaa ya kuwa kwenye Kamati ya Utendaji ya TFF.

Nabadala yake mgombea huyo alijibu viwili vya Mpanda na Katavi huku akishindwa vilivyo baki na kukiri kwamba havifahamu. #UchaguziTFF.

By Hamza Fumo

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW