Michezo

Dodoma: Mtoto wa mgombea TFF adakwa chooni na burungutu la hela

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amethibitisha kuwa jeshi la Polisi kwa kushirikiana na TAASISI ya kuzuia na kupamabana na rushwa TAKUKURU inamshikilia kijana mmoja kwa tuhumza ya kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa

Kijana huyo aliyejulikana kwa jina la Endru Kevela Yono ambaye baba yake ni miongoni mwa wagombea amekutwa chooni katika ukumbi wa mikutano wa St. Gaspar mjini Dodoma ambao ndiyo uchaguzi wa TFF unapofanyika akiwa na burungutu la laki tano huku akiwa amegawa katika mafungu ya shilingi elfu hamsini yakiwa tayari kwa kupatiwa baadhi ya wa jumbe ambao orodha ya majina yao yameandikwa

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa  akizungumza na Shirika la utangazi Tanzanai (TBC) amesema “Tumemkuta chooni ambako aliandaa mazingira kwamba wajumbe wanapo kwenda kule basi wapewe hizo bahasha kwahiyo hakuna ubishi ni swala la rushwa”, amesema.

Kamanda Mambosasa ameongeza kuwa “Niendelea kutoa wito na rai kwa wajumbe na wapambe wao waliyokuja kufuatilia shughuli hii, tulichoonya ndicho tunachokifanya yeyote ambaye atajaribu kuendelea kupuuza kujihusisha na vitendo hivi vya rushwa ajue hatakuwa salama kama alivyokuwa huyu kijana”.

“Huyu kijana sasa yupo mbaroni anaendelea kuhojiwa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na TAKUKURU kwahiyo niseme tu kwamba yeyote anayetaka kuendelea nkujihusisha na vitendo hivi hayupo salama nilisema hapo jana kuingia ni rahisi lakini utokaji ni shighuli”amesema kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents