Michezo

Dodoma: Wallace Karia rais mpya TFF

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) hatimaye limepata rais mpya ambaye ataliongoza kwa muda wa miaka minne kabla ya kufanyika tena uchaguzi Mkuu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi  wakili msomi, Revocatus Kuuli amemtangaza, Wallace Karia kuwa rais mpya wa TFF baada ya kupata jumla ya kura tisini na tano huku akiwaacha wapinzani wake mbali.

Katika matokeo hayo ya uchaguzi wajumbe wa TFF wamempitisha, Mulamu Nghambi kuwa makamu wa rais baada ya kupata jumla ya kura 25.

Hawa ndiyo baadhi ya wagombea na idadi ya kura walizo pata
URAIS

A: Wallace Karia  amepata jumla ya kura 95
B: Fredrick Mwakalebela  amepata kura 3
C: Emmanuel Kimbe amepata kura 1
D: Iman Madega amepata kura 8
E: Shija Richard amepata jumla ya kura  9
F: Ally Mayay amepata jumla ya kura 9

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents