Uncategorized

Dogo aliyeomba pambano na Floyd Mayweather ‘Money Man’ akiona chamoto ulingoni (+video)

Bondia wa Marekani, Floyd Mayweather maarufu kama ‘Money Man’ ameibuka na ushindi baada ya kumpiga vibaya Mjapan, Tenshin Asukawa kwenyepambano la ngumi lililofanyika nchini Japan.

https://www.youtube.com/watch?v=oydwbTnq6tE

Kwenye pambano hilo Mayweather aliandaliwa kitita cha dola za Kimarekani milioni tisa kwaajili ya kuzipiga na Tenshin Nasukawa pambano la raundi tatu.

Mara baada ya pigano hilo Mayweather amewashukuru mashabiki zake ‘’Kwanza kabla ya yote natanguliza shukrani zangu kwa Mungu kwa hiki kilichotokea, kwa tukio hili, timu yangu, Tokyo na nyie vijana wa Japan nawashukuru,’’ amesema Mayweather.

Kickboxer huyo aliyeamua kupigana mchezo wa boxer aliondoka ulingoni huku akimwaga machozi kwa kulia kutokana na kipigo alichokipata kutoka kwa Money Man.

Mayweather amempiga dogo huyo wa miaka 21 katika raundi ya kwanza dakika ya pili huku akianguka chini maratatu kabla ya mwamuzi kuamua kumpa ushindi Mmarekani huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents