Burudani

Dogo Janja achomoa kumdiss Harmonize

Msanii wa Bongo Fleva, Dogo Janja amesema ujumbe alioandika kwenye mtandao juzi haujamlenga Harmonize kama watu wengi wanavyodhani.

Hivi karibuni Dogo Janja kwenye mtandao wa twitter aliandika, “Raymond kanikonga nyoyo sana leo… yule Amber Rose angekaa hata kwenye category mjini hapa msingehema”.

Watu wengi waliamini ujumbe huo umemlenga Harmonize kwa kuwa nywele zake ameweka rangi na kufanana sawa na za Amber Rose. Lakini Dogo Janja amesema kimsingi Harmonize haitwi Amber Rose kwa sababu hata Amber Lulu ni Amber, hivyo hawezi kuliongelea zaidi.

“Kitu nachoweza kusema watu wamekuwa wakiishi kwa hisia lakini sijamlenga mtu kwa sababu hata Amber Lulu ni role model wa Amber Rose, kwa hiyo kama ni msingi ni Amber Rose,” Dogo Janja ameiambia XXL ya Clouds FM na kuongeza.

“Amber Rose ni mtu yeyote ambaye ameweka nywele brichi, sidhani kama ni yeye pekee yake ameweka hivyo, kuna Amber Lulu ameweka style hiyo, kuna Tunda, kwa hiyo kama msela ni Tunda au Amber Lulu fresh,” amesistiza Dogo Janja.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents