Burudani

Dogo Janja anazeeka vibaya, asaidiwe – Nedy music

By  | 

Msanii wa muziki kutoka label ya PKP ya Ommy Dimpoz, Nedy Music anaendelea kushambuliana na rapa Dogo Janja kutoka Tip Top Connection.

Nedy Music

Mzozo huo ulianza baada ya rapa huyo kujinadi kwamba yeye ni mkali wa kuvaa kuliko wasanii wote kauli ambayo ilipingwa na muimbaji huyo wa ‘Dozee’ kutoka PKP.

Akiongea na Bongo5 Jumatato hii, Nedy amedai Dogo Janja ni kama mzee ambaye anazeeka huku uwezo wake wa kufikiri ukipungua kila siku.

“Mimi nachoweza kusema ni kwamba Dogo Janja asaidiwe, ana zeeka vibaya kila siku anabadilika,” alisena Nedy “Uwezo wake wakufikiri unapungua kila siku, mimi ningewashauri ndugu zake wamsaidie kwa sababu anapotea,”

Aliongeza, “Pia Dogo Janja amefundishwa kuvaa na Madee hakuna asiyejua hilo, tena ananunua nguo za Manzese, hawezi kushindana na mimi labda ashindanishwe na densa wangu lakini siyo mimi mtoto wa mjini,

Nedy kwa sasa anafanya vizuri na wimbo, Dozee.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments