Burudani

Dogo Janja atoa somo katika uvaaji wake

By  | 

Msanii wa Bongo Flava, Dogo Janja ametoa soma katika uvaaji wake.

Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ‘Ukiavaaje Unapendeza’, ameimbia Dj Show ya Radio One kuwa watu wengi wamekuwa wakidhani ili mtu apendeze ni lazima awe na fedha nyingi kitu ambacho si kweli.

“Watu wamekuwa wakilinganisha muonekano wangu na fedha, ninachoamini kuvaa sio fedha nyingi sana ila kuvaa ni passion ya mtu, so kila mtu anavaa ndio maana nikasema ukivaje unapendeza kitu ambacho kipo watu wanavaa huwezi kutembea utupu hata siku moja,” amesem Dogo Janja.

Kabla ya kuachia ngoma yake “Ukivaje Unapendeza’ aliingia katika ubishani na watu wengi baada ya kujigamba kuwa yeye ndiye masanii anayeongoza kwa kupendeza Bongo.

By Peter Akaro

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments