Burudani

Dogo Mfaume alikuwa ana tatizo la uvimbe kichwani – Misana

Kifo cha msanii wa muziki wa Mchiriku, Mfaume Selemani maarufu kama  Dogo Mfaume, kimekuja ikiwa ni siku chache tangu Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla kutoa msaada kwa ajili ya matibabu ya uvimbe karibu na ubongo uliokuwa unamsumbua.

Dogo Mfaume enzi za uhai wake.

Dogo Mfaume aliyewahi kutamba na wimbo ‘Kazi Yangu ya Dukani ‘, amefariki leo (Jumanne) katika hospitali ya Taifa Muhimbili (MHN)  alipokuwa amelazwa akiendelea na matibabu.

Mmiliki wa kituo cha Pili Misana Back To Life sober house kinachotoa matibabu kwa waathirika wa dawa za kulevya, Pili Misana amesema Kigwangalla alitoa msaada huo baada ya fedha za matibabu kukosekana.

“Dogo Mfaume alikuwa akisumbuliwa na maradhi tangu mwanzoni mwa mwaka huu na baadaye iligundulika kuwa na uvimbe karibu na ubongo na hapo ndipo Naibu Waziri akatupatia msaada tukaanza matibabu Muhimbili,” amesema.

Amesema wiki hii Dogo Mfaume alikuwa amelazwa Muhimbili akisubiri kufanyiwa upasuaji Ijumaa.

“Kesho tulitakiwa twende hospitali kwa ajili ya kumtolea damu, lakini kwa bahati mbaya amefariki,”amesema.

Hii ni moja kati ya kazi zake ambayo ilifanya vizuri kipindi cha nyuma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents