Tia Kitu. Pata Vituuz!

Dogo wa miaka 19 avunja rekodi ya Messi, ashangilia kama Ronaldo, La Pulga akosa la kufanya

Kinda wa Real Madrid, Vinicius Junior usiku wa jana ameandika historia ya kuwa mchezaji wa kwanza mwenye umri mdogo zaidi kufunga goli kwenye mchezo wa El Clasico ndani ya karne ya 21 na kuvunja rekodi hiyo iliyokuwa inashikiliwa na mshambuliaji bora duniani, Lionel Messi ‘La Pulga’.

Vinicius Jr copied Cristiano Ronaldo's celebration after scoring in El Clasico on Sunday night

Mbrazil huyo, mwenye umri wa miaka 19 amefunga goli hilo la utangulizi dakika ya 71 dhidi ya Barcelona kwenye mchezo uliyomalizika kwa ushindi wa mabao 2 – 0 usiku jana siku ya Jumapili katika dimba la Bernabeu.

The Brazilian fired home the first goal as Real Madrid defeated Barcelona 2-0 at the Bernabeu

Vinicius Junior amefunga goli hilo kwenye El Clasico akiwa na umri wa miaka 19 na siku 233 wakati waka Lionel Messi ambaye alikuwa na shikilia rekodi hiyo akiwa amefunga alipokuwa na umri wa miaka 19 na siku 259.

Kwa maana hiyo basi Mbrazil huyo anakuwa mchezaji wa kwanza mwenye umri mdogo zaidi kufunga bao kwenye mechi ya Real Madrid na Barcelona maarufu kama El Clsico.

Baada ya kufunga goli, Vinicius Jr alikwenda mpaka kwenye kibendera cha kona na kushangilia kama Ronaldo kwa kuruka juu na kutanua mikono pamoja na miguu, mchezaji ambaye ameweka historia kubwa ndani ya Real Madrid huku Mreno huyo aliyehamia Juventus akishuhudia tukio hilo katika Uwanja wa Bernabeu na kufurahishwa na kitendo hicho hali iliyopelekea kumpigia makofi akiwa jukwaani.

Wakati baadhi ya mashabiki pamoja na kamera za TV  ziliweza kumnasa jukwaani akiwa anashangili.

Kipande cha Video kikimuonesha Ronaldo mwenye kizibao cheusi akishangilia goli lililofungwa na Vinicius Jr.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW