Burudani

Dokta Mwaka kuja na semina ya afya kwaajili ya wasanii na vijana kwa ujumla

Daktari wa masuaa ya afya ya uzazi na mengine, Dr. Mwaka ameandaa semina maalumu ya kutoa elimu ya afya kwa ajili ya wasanii na vijana nchini, ikiwa na lengo la kutoa elimu ya uzazi kwa vijana.

IMG_9093
Dr Mwaka na Mkurugenzi Mkuu wa THT, Ruge Mutahaba wakiongea na waandishi

IMG_9098
Dr Mwaka akiongea na waandishi wa habari

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu semina hizo, Mkurugenzi Mkuu wa THT, Ruge Mutahaba alisema kituo cha THT ambacho kimekuwa msitari wa mbele katika kukuza vipaji kinaamini pia afya za vijana hao ni jambo muhimu katika kufikia ndoto zao hasa katika matatizo ya mfumo wa uzazi ambalo limekuwa tatizo kubwa sana kwa vijana wengi.

‘Kimsingi hata uwe na kipaji namna gani kama hauna afya njema huwezi kufikia ndoto zako hata kidogo, na ndio maana tumeona tushirikiane na Dkt. Mwaka ili kuwapa elimu wasanii wote walio chini ya THT lakini pia wengine wote hapa nchini,” alisema Ruge.

IMG_9100

Naye Dkt. Mwaka akizungumza na waandishi wa habari alisema mara nyingi matatizo ya kiafaya kwa vijana yanachochewa kwa kiasi kikubwa na aina ya maisha wanayoishi (lifestlye).

‘Kama vijana, lakini pia wasanii wana nafasi kubwa ya kupata matatizo ya kiafya kwa sababu tu ya aina ya kazi yao lakini pia watu wengi wanaowazunguka’ alisema Dkt Mwaka.

IMG_9087
Shilole akiongea na waandishi wa habari

Semina hizo ambazo zitafanyika tarehe 18 ya mwezi huu wa tatu katika Ukumbi wa Little Theatre, Masaki hapa jijini Dar es Salaam, zitajumuisha vijana na wasanii wa muziki, filamu pamoja na michezo kama kundi la kwanza.

‘Wasanii ni mabalozi, na tunaamini kwa wao kuonyesha mfano wa kuishi maisha yenye afya njema tuna hakika wataweza kuwafikia vijana wengi zaidi hapa nchini hasa katika hili tatizo la uzazi kwa vijana’ alisisitiza Dkt Mwaka.

THT ilianzishwa mwishoni mwa mwaka 2005 kwa lengo la kuwasaidia vijana wenye vipaji, lakini wasio na uwezo wa kujiendeleza wenyewe, kwenye sekta ya sanaa hapa nchini, na toka wakati huo kituo kimekuwa na mafanikio makubwa na mchango wa pekee kwenye kukuza sanaa ya muziki nchini.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents