Donald Trump aporomoka orodha ya matajiri duniani, Bill Gates ashushwa nafasi ya kwanza

Jarida la Forbes limetoa orodha ya watu matajiri duniani, Rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump ameporomoka kwa nafasi takribani 200.

Trump ametajwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 3.1 huku akishika nafasi ya 766 ambayo inashikiliwa na watu wengine takribani 25.

Utajiri wa Rais huyo wa Marekani umetajwa kushuka kwa dola milioni 400 ambapo kwa mwaka jana alitangazwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 3.5.


Mwanzilishi wa kampuni ya Amazon, Jeff Bezos

Katika orodha hiyo mwanzilishi wa Amazon, Jeff Bezos anashika nafasi ya kwanza akiwa na utajiri wa dola bilioni 112 akimbwaga Bill Gates anayeshika nafasi ya pili akiwa na utajiri wa dola bilioni 90.

Wakati huo huo mwanzilishi wa mtandao wa Facebook, Mark Zuckerberg anashika nafasi ya tano akiwa na utajiri wa dola bilioni 71. Aliko Dangote kutoka Afrika anashika nafasi ya 100 akiwa na utajiri wa dola bilioni 14.1.

Naye Mohammed Dewji wa Tanzania anashika nafasi ya 1561 akiwa na utajiri wa dola bilioni 1.5.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW