Habari

Donald Trump azindua rasmi kampeni za kutetea kiti chake cha Urais 2020

Rais wa Marekani Donald Trump amezindua rasmi kampeni za kutetea kiti chake cha urais katika uchaguzi utakaofanyika mwakani 2020.

TRUMP

Trump amewataka wafuasi wake wahakikishe “timu yake inasalia ilipo” kwa miaka minne zaidi. Rais huyo anayetokana na chama cha Republican alitangaza uamuzi wake huo mbele ya maelfu ya wafuasi wake kwenye mkutano wa hadhara Florida, huku akilitaja jimbo hilo kuwa “makazi yake ya pili.”

Trump alitumia mkutano huo kuekeza mashambulizi kwa chama cha Democrats, akiwatuhumu wanachama wake kwa kujaribu “kuichanachana vipande

Hata hivyo, kura za maoni za awali zinaonesha kuwa Trump yupo nyuma ya wagombea kadhaa ambao wanaweza kusimamishwa na chama cha Democrats.

Aliungana jukwaani na mkewe Bi Melania, ambaye amesema kuwa atakuwa mwenye furaha kuendelea kuwa Mke wa Rais mpaka mwaka 2024.

“Leo hii nasimama mbele yenu kuzindua kampeni zangu za awamu ya pili kama rais wa Marekani,” Trump amewaambia wafuasi wake. ” Nawahakikishia kuwa sitawaangusha.”

Florida ni moja ya majimbo magumu ya kisiasa na Trump lilinyakua kwa ushindi mwembamba mwaka 2016.trump

 

“Tutaendelea kuifanya Marekani kuwa imara zaidi,” amesema kwenye mkutano huo uliofanyika Jumanne usiku kwa saa za Marekani.

Baadhi ya wafuasi wake walikuwa wakisubiria kumuona kwa siku moja kabla.

Maandamano ya kumpinga Trump yalifanyika katika eneo karibu na alipofanya uzinduzi wake wa kampeni.

Trump amesema nini?

Katika hotuba yake ya dakika 80, Trump alirejelea baadhi ya mambo ambayo yalimhakikishia ushindi katika kampeni za mwaka 2016.

Ameendelea kuahidi kubana mbavu uhamiaji haramu, siku moja baada ya kuchapisha kwenye mtandao wake wa Twitter kuwa mamlaka za uhamiaji hivi karibuni zitawarudisha makwao mamilioni ya wahamiaji haramu.

“Tunaamini nchi yetu inatakiwa kuwa ni sehemu salama kwa wananchi wafuatao sheria, sio kwa wahamiaji haramu wahalifu.”

Pia amewashutumu viongozi wa Democrats kwa kutaka kuwahalalisha wahamiaji haramu ili kuongeza idadi ya wapiga kura wao na kusema “wanataka kuharibu nchi yetu.”

Trump amewaita wapinzani wake kama genge la wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kushoto. “Kumchagua kiongozi yeyote wa Democrat mwaka 2020 ni kuchagua kunyanyua siasa kali za kijamaa na kusambaratisha ndoto ya Marekani,” aliiambia hadhara.

Pia amesifu ukuaji wa uchumi, akaukashifu uchunguzi dhidi yake maarufu kama Ripoti ya Muller, amabo uliangalia iwapo alishirikiana na Urusi kwenye kampeni zake za mwaka 2016, na kusema taarifa za habari kuhusu uchunguzi huo zilikuwa ghushi.

Nini kilitokea kabla ya hotuba yake?

Maelfu ya wafuasi walikusanyika nje ya eneo , wengine waliweka kambi eneo la Amway huko Orlando tangu mapema Jumatatu asubuhi.

Trump mwenyewe alidai kuwa idadi ilikua ni maelfu siku mbili kabla hata hajafika katika eneo hilo.Supporters waiting outside arena holding flags, MAGA hats

Wafuasi wa Trump wakimsubiria

Chombo cha habari cha CBS kimetoa taarifa kuwa wapiga kura wengi waliokua katika foleni, wametaja suala la uchumi na uhamaiaji kama mambo makuu ambayo Trump anatakiwa kuyaongelea wakati wote wa kampeni zake.

Waandamanaji pia walihudhuria baada ya kufanikiwa kwa harambee yao kupitia tovuti ya GoFundMe, pulizo linaloakisi muonekano wa Trump akiwa mtoto lilielea katika anga ya London pia wakati wa ziara ya hivi karibuni ya umoja wa ulaya lilionekana.

Video katika mitandao ya kijamii kutoka eneo la tukio zimewaonesha kundi la msimamo mkali la mrengo wa kulia wakizuiwa na polisi walipotaka kuingilia maandamano ya wanaompinga Trump

Mtihani wa Trump kuwasawishi Wamerekani

Na Anthony Zurcher

Mwandishi wa BBC Amerika Kaskazini

Siku ya jumanne jioni huko Orlando, Florida, Donald Trump alianza Rasmi kampeni zake za kugombania muhula wa pili wa Urais.

Hakuna mtu aliyeshangazwa, tayari watu walijua kuwa atagombea muhula wa pili, alijaza fomu yake ya 2020 mara baada ya kuapishwa Januari 2017 na tangu hapo amekua akipiga kampeni zake mara kwa mara katika majimbo mbalimbali.Opposition Groups Protest President Donald Trump Outside Rally Announcing His Re-Election Candidacy

Wapinzani wa Trump

Na siku ya Jumanne huko Florida, moja ya jimbo kubwa la ushindani wa uchaguzi,jimbo ambalo ni lazima Rais ashinde uchaguzi wa 2020, siku hiyo ilikua sio kuhusu kutoa taarifa yake ya kugombea muhula wa pili bali ilikua ni kwa namna gani ataweza kushinda.

Tukio lilikua ndio mara ya kwanza Trump anatoa taarifa yake wazi wazi ya kugombea muhula wa pili katika uwanja wa unao beba watu elfu ishirini, mbele ya kundi la Maelfu ya wafuasi waliokua wakishangilia kwa kelele za hali ya juu huku wakiwa wamevalia kofia nyekundu.

Mgombea wa Demokratiki Bernie Sanders alituma ujumbe Twitter uliosema kuwa ”trump anaishi katika ulimwengu wa kufikirika”

”kazi yetu ya msingi ni kuhakikisha tunamshinda Rais hatari Zaidi katika historia ya nchi hii” alisema Bernie Sanders.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents