Michezo

Done Deal: Mourinho huyo ndani ya Manchester United

Baada ya drama ya muda mrefu hatimaye Jose Mourinho Ijumaa hii anatarajiwa kusaini mkataba wa kuifundisha Manchester United.

Jose-Mourinho-United-main

Mourinho ambaye tangu amefukuzwa timu ya Chelsea amekuwa hana timu anatarajia kusaini mkataba huo na kuchukua mikoba ya aliyekuwa kocha wa Manchester United, Louis Van Gaal ambaye amefukuzwa klabuni hapo wiki iliyopita baada ya kufanya vibaya kwenye ligi kuu ya Uingereza lakini alifanikiwa kuiwezesha timu hiyo kuchukuwa kombe la FA.

Kwa mujibu wa Skysport, mazungumzo kati ya wakala wa Mourinho, Jorge Mendez na uongozi wa timu ya United yanaendelea vizuri huku kocha huyo akiwa tayari ameshakubaliana masharti binafsi.

Aidha imeripotiwa kuwa Mourinho amepanga kutua na wachezaji kadhaa kwenye timu hiyo ambao ni Saul Niguez, Willian wa Chelsea na Higuain huku wakiendelea kufanya mazungumzo na Zlatan Ibrahimovic aliyemaliza mkataba wake na PSG.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents