Burudani

Doreen Mashika ameremeta na ‘Fashion Night In’

Katika jioni ya umaridadi na matarajio makubwa, mbunifu wa mavazi, Doreen Mashika amewageukia mashabiki wake wa bara na kuwashangaza katika usiku uliojulikana kama ‘Fashion Night In’ uliokuwa mjumuhisho wa rangi na miundo inayofaa kuigwa.

DM (23)

Mbunifu huyo aliyewahi kushinda tuzo mbalimbali duniani alionyesha toleo jipya la mavazi yake yaliyojulikana kama “spring/summer 2015”.
Pamoja na utajiri wa vipaji alivyonavyo watazamaji walipata kuona mitindo ya kipekee, uzoefu mpya na msisimko ambayo ni alama mahususi ya Doreen Mashika Zanzibar (DMZ).

Hii halikuwa tukio la kukosa lililohudhuriwa na wageni wa kimataifa kutoka maeneo mbalimbali pamoja na wanamitindo, wabunifu, watu mashuhuri na kwa ujumla wapenzi wa mitindo.

DM (31)

Diva wa ‘Fashion Night In’, Doreen Mashika alifungua onesho kwa kuonesha miundo mipya ya mtindo. Akitoa maoni juu ya mwelekeo wake wa ubunifu Doreen Mashika anasema, “kama mbunifu najaribu kufikiri nje ya boksi na kukata minyororo ya mtazamo na mitindo iliyozoeleka, naamini ili bidhaa iweze kukubalika na kukumbukwa kweli inapaswa kuleta changamoto katika fikra za kila mmoja.”

DM (26)

Onesho hilo ililetwa ki ubora zaidi na mkurugenzi wa uzalishaji Rob Soar kutoka London na kuwekewa muendelezo na timu yenye vipaji lukuki kutoka Dar es Salaam na Nairobi. Utanuzi huu wa lebo ya DMZ umewashangaza wafwatiliaji kwa kuchukua muelekeo mpya katika Mitindo unaozidi kuimarika na kuelekea ulimwenguni kote.

DSC00620-01

Katika sekta hii ndogo na inayobadilika Doreen Mashika anakuwa kama mwanga elekezi kwa wabunifu wenzake kutokana na kujituma kwa bidii na utofauti bila kusahau utamaduni wake wa Kiafrika.

Kuhusu Doreen Mashika

Doreen Mashika alizaliwa na kukua nchini Tanzania, alisoma na kufanya kazi nchini Uswiss.

Alianza kazi katika sekta ya fedha akiwa Uswisi. Akijikita kwenye bidhaa za kifahari huko ndipo alipoanzia kupenda maswala mtindo na ubunifu. Akiongozwa kwa hisia utamaduni na utajiri uliopo barani Afrika, alirejea Tanzania na kukaa Zanzibar na kuazisha kampuni yake.
Hivi sasa, anamiliki duka lenye bidhaa zinazovutia kimataifa. Ameunda bidhaa za kipekee na kisasa zenye mchanganyiko wa mitindo ya kimagharibi na vifaa vya jadi.

Bidhaa za DMZ zinavutia rangi, mahiri na ni maridadi. Bidhaa hizo ni pamoja na viatu, mikoba, vito na nguo zinazotengenezwa kwa kutumia nguo za jadi za Kiafrika kama vile Kanga, vitenge na turubai. Katika kubuni mifuko na viatu, Mashika anashirikiana na vikundi vya wanawake kutoka vijijini wanaotengeneza vitu hivyo kwa kutumia mikono, na pia kwa kutumia mbinu za jadi za kiafrika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents