Michezo

Dortmund yachoshwa na Aubameyang sasa ruksa (Picha)

Klabu ya Borussia Dortmund ipo tayari kuachana na straika wake Pierre-Emerick Aubameyang ambaye anawaniwa na timu za Liverpool pamoja na Chelsea.

Straika wa klabu Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang

Dortmund italazimika kumuuza Aubameyang ili kuepuka hasara ya kuondoka bure kwa mchezaji huyo, haya yanakuja baada ya timu hiyo kutoka sare ya mabao 4-4 katika mchezo wao wa derby dhidi ya Schalke katika ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani.

Mara baada ya mchezo huo meneja wa kikosi hicho, Peter Bosz amesema kufuatia utovu wa nidhamu unaoonyeshwa na straika huyo wa kimataifa wa Gabon  muda wa kubaki ndani ya klabu hiyo umekwisha.

Mlinda lango wa Dortmund, Roman Weidenfeller amesema meneja wa kikosi hicho, kachoshwa na ujinga unaofanywa straika huyo nakusema kuwa amepoteza kilakitu.

Liverpool na Chelsea ni klabu mbili ambazo zimeonesha nia za kutaka kumsajili mshambuliaji huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents