Michezo

Dortmund yathibitisha mchezaji wake kwenda Manchester United

Timu ya Borussia Dortmund imethibitisha kuwa mchezaji wake Henrikh Mkhitaryan anakwenda Manchester United.

Dort

Kupitia akaunti ya Twitter, timu hiyo imeandika ujumbe unaoeleza kuwa mchezaji huyo anaelekea United kutokana na kukubaliana kwa masharti ya kumsajili. Manchester United inatajwa kuwa imetumia paundi milioni 26 kuishawishi Dortmund ili kumwachia mchezaji huyo raia wa Armenia na kumfanya kuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa chini ya kocha Jose Mourinho.

Mkhitaryan amefanikiwa kuichezea timu ya Dortmund jumla ya mechi 88 na kufunga magoli 23.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents