AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Dotnata atoa usia kwa wasanii wakongwe

dotnata

 

 Dotnata amesema lazima kwanza tukubali kwamba mwanzo mgumu, lakini isiwe sababu ya kutoendelea mbele. amesema kwa sasa wahindi, wamefanikiwa kulifikisha soko la filamu mbali kwa ndani na nje ya nchi lakini kwa sasa ni muda wa watanzania wenyewe kulishika soko hilo.

aidha amedai kwamba  yeye tayari ameshaanzisha kundi la Maigizo la Dotnata Entertaiment, pia ameanzisha kampuni ya utengenezaji wa filamu ya Dotnata Produiction, na pia kwa sasa anakampuni ya Usambazaji wa kazi za filamu za wasanii.

 amesema mwanzo alikuwa ameingia hasara kwakuwa alikuwa anaanza, lakini kwa sasa mambo yanamwendea vizuri, kwakuwa soko watu wameshaanza kulijua.

Anasema ndivyo hivyo kuna wasanii wanauza sana, tena Cd zao zinatoka, lakini wanakuwa na maisha duni kwakuwa uuzaji wa kazi zao ni za kunyonywa sana, hivyo ni bora wakubali hasara za muda mfupi ili baadaye waje kupata faida kubwa.

Dotnata pia amesema kwa mwaka wa 2012, anakuja na filamu yake ya kwanza ambayo atamshirikisha King Majuto ambayo itaitwa Ila. anasema hiyo itakuwa ni filamu ya kwanza ya Majuto kuigiza sliasi tangu alipoanza kuigiza filamu Duniani.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW