Michezo

DR Congo mabingwa wa mashindano ya CHAN

Timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametwaa ubingwa wa kombe la Chan baada ya kuichapa Mali kwa mabao 3-0.

DR-Congo

Mabao ya washindi ya Congo yalifungwa na Meshak Elia aliyefunga bao mbili wakati Jonathan Bolingi alifunga goli jingine kukamilisha ushindi wa DR Congo.

Mwaka 2009 DR Congo ilichukua kombe hilo kwa mara ya kwanza kwa kuifunga Ghana kwa magoli 2-0 kwenye mchezo wa fainali.

Kwenye mashindano ya mwaka huo Tanzania pia ilishiriki michuano hiyo lakini ilitolewa kwenye hatua ya makundi.

DR Congo imechukua kitita cha dola za Marekani 750,000 wakati mshindi wa pili ambayo ni timu ya Mali yenyewe ikiondoka na dola za Marekani 400, 000 huku mshindi wa tatu timu ya taifa ya Ivory Coast ikijishindia dola 250,000

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents