Burudani

Dr. Dre kuchangia $10m katika ujenzi wa shule ya sanaa

By  | 

Mtayarishaji wa muziki na rapper wa Marekani, Dr. Dre ameahidi kuchangia kiasi cha dola milioni 10 kwa ajili ya kujenga shule ya sanaa Compton High School.

Kwa mujibu wa mtandao wa Los Angeles Times, rapper huyo amesema ameamua kufanya hivyo kwa ajili ya kuwasaidia vijana waweze kuwa wabunifu kwa njia ambayo itasaidia kuendeleza elimu yao.

“My goal is to provide kids with the kind of tools and learning they deserve. The performing arts center will be a place for young people to be creative in a way that will help further their education and positively define their future,” amesema Dre.


Mfano wa shule ambayo Dr. Dre anampango wa kujenga

Inadaiwa kuwa ujenzi wa shule hiyo unatarajiwa kuanza kufanyika mwaka 2020.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments