Burudani

Dr. Jose Chameleone aipeleka ‘Badilisha Tour’ Marekani, apata nafasi ya kutembelea kaburi la Bruce Lee!

Mkali kutoka Uganda Joseph Mayanja maarufu kama Dr. Jose Chameleone yuko katika ziara ya kimuziki nchini Marekani aliyoipa jina la ‘US Badilisha Tour’.

dr Jose

Mbali na show zilizompeleka huko, hit maker wa ‘Badilisha’ Chameleone pia ameweza kutembelea kaburi la muasisi na muigizaji maarufu wa filamu za karate, mwenye asili ya uchina na Marekani marehemu Bruce Lee aliyefariki mwaka 1973, ambalo liko karibu na kaburi la mwanae Brandon Lee aliyefariki mwaka 1993.

Ziara ya Chameleone nchini Marekani imekuja baada ya kuandika historia nyingine nchini Uganda katika ‘Badilisha Concert’ takribani wiki 3 zilizopita ambayo ilikuwa na mafanikio makubwa.

Akiwa nchini humo mpaka sasa amekwisha fanya onesho moja katika jiji la Los Angeles, na Jumamosi (June 1) anategemea kufanya show Seattle itakayofuatiwa na show nyingine (June 7) Maine.

Miji mingine iliyo katika ratiba ya ‘Us Badilisha Tour’ ni pamoja na Washington D.C (June 8) , Phonix AR (June 15), na atamalizia show yake ya mwisho huko jimboni Illinois (June 22).

Chameleone mwenye miaka 34 na baba wa watoto wawili (Alfa & Abba) aliondoka nchini Uganda May 23 akielekea Marekani ambako atakaa mwezi mzima katika ziara yake ya Badilisha ambayo amekuwa akiwa update mashabiki wake kupitia ukurasa wake wa facebook kuhusiana na ziara hiyo. ‘Badilisha’ ni jina la hit song inayobeba album yake ya 14 iliyopewa jina hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents