Burudani

Drake amchana Breezy: ‘Mwanamke ampendaye alijileta na nikafanya kile mwanaume wa kweli angefanya

Hivi karibuni Chris Brown amekuwa akimzungumzia sana Drake kwenye interview anazofanya na sasa Drake amefunguka kwa upande wake. Miaka kadhaa iliyopita wakati Chris & Rihanna walikuwa wameachana, Rih alidaiwa kuanzisha uhusiano na Drake na hawajawahi kukanusha.

tumblr_lj1qa4nUNO1qfh5ofo1_500

Kwakuwa Drake na Chris walikuwa washkaji, kitu hicho kiliwafanya wawe na beef kiasi cha mwaka jana kupigana kwenye club ya usiku. Rapper huyo wa “Started From the Bottom” jana alifanya mahojiano na Elliot Wilson na kuzungumzia issue yake na Chris.

Kwenye interview hiyo Drake alimuita Chris kuwa ni mtu asiyejiamini kwakuwa (Drake) muziki wake ni bora zaidi na kwakuwa Rihanna aliingia kwenye anga zake.

“Kwa chombo chochote cha habari huko nje, msiniulize lolote kuhusu huyo jamaa nikija huko. Mwacheni. Msitekwe na kutojiamini kwake. Kutokujiamini kwake ni sababu natengeneza muziki mzuri kumzidi, nafanya vizuri kuliko yeye. Katika wakati mmoja wa maisha mwanamke anayempenda alijileta kwangu na nikafanya kile mwanaume wa kweli angefanya na kumtreat kwa heshima.

Msikilize zaidi hapa:

[soundcloud url=”http://api.soundcloud.com/tracks/87638156″ params=”” width=” 100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents