Burudani

Drake asample wimbo wa Black Coffee kwenye album ya More Life

Drake amesample wimbo wa Dj wa Afrika Kusini, Black Coffee ‘Superman’ kwenye album yake mpya More Life.

Wimbo wa Drake kwenye album hiyo unaitwa Get It Together aliowashirikisha Black Coffee na Jorja Smith. Awali kwenye wimbo wa Black Coffee, Superman msanii aliyeimba ni Bucie ambaye naye atachukua mkwanja mrefu kutokana na maishari yake kutumika.

Bucie ametajwa kama mmoja wa waandishi wa wimbo huo. Wapo watu nchini Afrika Kusini ambao wamekosoa kutoshirikishwa kwa Bucie kwenye wimbo huo na kufanya jina lake litrend kwenye Twitter.

Lakini Bucie halalamiki kwasababu ametajwa rasmi kama mmoja wa waandishi na atalipwa mrabaha wake kila wimbo huo ukichezwa.

“It is a great achievement and says a lot about my writing skills,” amesema Bucie.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents