Burudani

Drake athibitisha kuachia ngoma mpya leo, adai yupo mbioni kukamilisha albamu yake

By  | 

Baada ya ngoma ya God’s Plan kufanya vizuri hasa idea ya video yake huku ikiwa imetazamwa zaidi ya mara milioni 334 kwenye mtandao wa YouTube, Drake amethibitisha kuwa anaachia ngoma mpya usiku wa leo (Ijumaa).

Rapper huyo amesema hayo wakati alipokuwa jukwaaani mjini Toronto ambapo pia amedai sababu ya kufika huko ni kwa ajili ya kumalizia albamu yake.

Sababu ya mimi kuwa hapa usiku ni kwa sababu nimerudi kumalizia albamu yangu. Ninaachia ngoma mpya kesho usiku, kama tu utapata muda,” amesema Drake.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments