Burudani ya Michezo Live

Drake atoa ya moyoni baada ya kuzomewa na mashabiki hadi kupelekea kushuka jukwaani – Video

Drake atoa ya moyoni baada ya kuzomewa na mashabiki hadi kupelekea kushuka jukwaani - Video

Waliohudhuria katika Tamasha la Camp Flog Gnaw Los Angeles iliyoanzishwa na Tyler, lilizua gumzo Jumapili usiku kwani Kila mtu alitaka kumjua msanii kinara ‘headliner’ wa tamasha hilo atakuwa nani na Wengi walitarajia kumuona Frank Ocean na Jina lake ndio wote walikuwa wanalitaja walitarajia kumuona sana kwamba atatokea.

Lakini cha kushangaza zaidi msanii kinara ‘headliner’ wa tamasha hilo akatokea Drake kitu ambacho kilionyesha watu hawakufurahishwa na ujio wa Drake kama msanii kinara ‘headliner’ wa tamasha hilo hivyo zilizuka kelele za kumzomea hadi kupelekea kushuka ndani ya jukwaa.

Lakini baada ya tukio hilo Drake amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kuzomewa na mashabiki wa tamasha la Camp Flog Gnaw, kupitia ukurasa wake wa Instagram na kusema.
“Mchezo umegeuka, nimesaini mkataba wa miaka 10 kutumbuiza katika tamasha la Camp Flog Gnaw, naombeni radhi watoto tutaonana kila mwaka hadi wote mtakapofikisha miaka 30” alimalizia kwa kuweka emoji ya kucheka.

Baada ya kelele hizo za kuzomewa, Drizzy aliamua kuiacha steji na kuondoka kabla hata ya kumaliza muda wake.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW